Latest Movie :

Mechi ya Yanga, Simba yaingiza milioni 427

IMG_0097

Mechi ya Yanga, Simba yaingiza milioni 427

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba iliyochezwa (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 427,271,000.
Washabiki 49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5 ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.
Kwa upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 1,000 kwa kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo sh. 24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh. 17,471,311.07, DRFA sh. 10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh. 100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh. 71,341,186.86.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. KISOKA ZAIDI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger