Latest Movie :

MZUNGUKOO WA TANO LIGI KUU BARA

Ligi Kuu Logo
Mechi za mzunguko wa tano wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara zitachezwa wikiendi hii kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Mabingwa watetezi, Azam watarudi nyumbani kwao, Azam Chamazi Complex kuwakaribisha JKT Ruvu. Azam wapo kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha pointi kumi sawa na Mtibwa Sugar. JKT Ruvu walioshinda mechi ya kwanza wiki iliyopita wana pointi nne wakiwa nafasi ya kumi.
Jijini Mbeya, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Simba kwenye uwanja wa Sokoine. Prisons wataingia katika pambano wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu. Simba wanaingia katika mchezo huo, ambao ni wa kwanza kucheza ugenini msimu huu, wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kuambulia sare nne mfululizo kwenye mechi za mwanzo za Ligi.
Maafande wa Polisi Morogoro watakuwa ugenini katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi kuwavaa wenyeji Ruvu Shooting.Kikosi cha kocha Tom Olaba kitaingia kwenye mchezo huo kikijivunia ushindi mnono wa ugenini dhidi ya Ndanda kilichoupata kwenye mzunguko wa nne.
Ndanda waliopanda daraja msimu huu watabaki nyumbani kuwakaribisha JKT Mgambo wanaoshika mkia kwenye msimamo.
Mjini Shinyanga, wageni wa ligi, Stand United watapambana na Yanga. Stand United inaoonekana kuimarika baada ya kuanza ligi kwa kupokea kipigo kikali kutoka kwa Ndanda kabla ya kujirekebisha na kupata matokeo mazuri kwenye mechi tatu za ugeni. Kwa upande wa Yanga, watakuwa wakisaka ushindi ili kuweza kuwasogelea vinara Azam na Mtibwa Sugar.
Kagera Sugar inayoshikilia nafasi ya tano itacheza mechi nyumbani kwa mara kwanza msimu dhidi ya Coastal Union iliyoonesha mwenendo mzuri msimu huu.
Mechi ya kukamilisha mzunguko wa nne itachezwa Jumapili kwa Mbeya City kuvaana na Mtibwa Sugar walioanza msimu kwa kasi nzuri. Mtibwa walishinda mechi tatu mfululizo kabla ya kubanwa mbavu na Polisi Morogoro wiki iliyopita. Wenyeji Mbeya City watahitaji kushinda kurejesha furaha ya mashabiki wao baada ya kufungwa na Azam wiki iliyopita.
Matokeo kamili ya Mzunguko wa nne:
Yanga 0-0 Simba
Prisons 1-2 JKT Ruvu
Ndanda 1-3 Ruvu Shooting
Coastal Union 2-0 JKT Mgambo
Kagera Sugar 0-0 Stand United
Mbeya City 0-1 Azam
Polisi Morogoro 0-0 Mtibwa Sugar
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. KISOKA ZAIDI - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger